KILIMO BORA CHA ALIZETI
Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga,
Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili
hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
Kuchagua aina bora ya mbegu
• Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta.
• Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.
KUWEKA MBOLEA
• Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.
KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA;
UKAGUZI
• Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupanda. Wakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25. Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu.

DALILI ZA ALIZETI ILIYOKOMAA
• Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi.
• Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia.
UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UBEBAJI
Vifaa vya kuvunia na kubebea kutoka shambani
• Kisu
• Vikapu
• Magunia
• Matenga Vifaa vya kukaushia
• Maturubai
• Mikeka
• Kichanja bora Vyombo vya usafiri kutoka shambani
• Matoroli
• Matela ya matrekta
• Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama
• Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisu. Pia mashine (combine harvester) hutumika kuvunia alizeti katika nchi zinazolima alizeti kwa wingi. Masuke ya alizeti huwekwa kwenye vikapu ambavyo hutumika kusomba alizeti ndani ya shamba. Kisha alizeti hufungashwa kwenye magunia na kusafirishwa hadi nyumbani tayari kwa kukausha.

KUKAUSHA
Kuna hatua mbili za kukausha alizeti; kukausha
masuke na kukausha mbegu za alizeti. Kukausha masuke
• Masuke hutandazwa kwenye kichanja bora katika kina
kisichozidi sentimita 30 ili yaweze kukauka vizuri.
• Vilevile huweza kutandazwa kwenye maturubai, mikeka au
sakafu safi.
• Lengo la hatua hii ni kukausha masuke ya alizeti ili
kurahisisha upuraji. KUPURA Upuraji hufanyika baada ya kuhakikisha kuwa masuke
ya alizeti yamekauka vizuri. Masuke ya alizeti hupurwa kwa kutumia mikono ambapo
mbegu hutenganishwa kwa kupiga masuke taratibu kutumia mti. Ni muhimu kupiga
masuke taratibu ili kuepuka kupasua mbegu
. • Pura kwenye kichanja bora, maturubai au mikeka.
KUKAUSHA MBEGU
• Mbegu za alizeti hukaushwa juani kwa
kutandazwa kwenye vichanja bora, maturubai, mikeka au sakafu safi.
• Tandaza mbegu katika kina kisichozidi sentimita 4 ili
ziweze kukauka vizuri.
• Lengo la hatua hii ni kukausha mbegu baada ya kupura
ili kufikia kiwango cha unyevu kinachotakiwa kwa hifadhi salama ambacho ni
asilimia 8.
JINSI YA KUTAMBUA MBEGU ZILIZOKAUKA VIZURI
Kufikicha mbegu
• Mbegu zilizokauka maganda yake hutoka kwa
urahisi zinapofikichwa. Kumimina kwenye chombo kama
debe
• Mbegu zilizokauka hutoa mlio mkali zinapomiminwa kwenye
vyombo hivyo.
• Mbegu zilizokauka hung’ara Kutumia kipima unyevu.
• Mbegu zilizokauka vizuri kipimo huonyesha asilimia 8
. KUPEPETA NA KUPEMBUA
Kupepeta na kupembua hufanyika ili kuondoa
takataka kama vile mawe, wadudu, mapepe, mbegu
zilizooza au kupasuka. Mbegu za alizeti hupepetwa kwa kutumia ungo au mashine
zinazoendeshwa kwa mkono, injini au umeme. Mashine hizi zina uwezo wa kupepeta
na kupembua kilo 60 hadi 350 kwa saa kutegemea aina ya mashine na ukubwa wa
mashine yenyewe
KUHIFADHI
Alizeti iliyopurwa huhifadhiwa katika hali ya kichele kwenye
maghala bora, yaani vihenge, sailo au bini. Alizeti ya kuhifadhi kwenye maghala
ya nyumba ifungashwe kwenye magunia na ipangwe kwenye chaga kwa kupishanisha. Ili kurahisisha kazi ya kukagua ghala, acha nafasi ya
mita moja kutoka kwenye ukuta. Ziba sehemu zote za ghala ili kuzuia panya
kuingia. Panya hupenda sana
kula punje za alizeti, na husababisha upungufu mkubwa wa punje ambao
husababisha upotevu wa asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya hifadhi.
Asilimia ya upotevu inaweza kuwa kubwa zaidi kutegemea idadi ya panya na
upatikanaji wa vyakula vingine kwa wakati huo. Matumizi ya Mbegu za Alizeti
Mbegu za alizeti hasa zenye mistari zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa au
kukaushwa. Pia zinatumika katika utengenezaji wa mikate. Mbegu za alizeti
husindikwa kupata bidhaa ya mafuta.
KUSINDIKA MBEGU ZA ALIZETI KUPATA MAFUTA
Vifaa
• Mashine ya kukamua mafuta
• Chujio safi
• Ndoo
• Vifungashio
• Sufuria
• Mizani Malighafi
• Mbegu za alizeti
• Maji
• Chumvi
NJIA YA KUKAMUA MAFUTA
• Chagua mbegu bora za alizeti
• Zianike kwenye jua kwa muda wa saa 1 hadi 2
• W eka kwenye mashine ya kukamulia ya daraja au Ram
• Kamua mafuta
• Chuja mafuta kwa kitambaa au chujio safi
• Pima mafuta yaliyokamuliwa.
• Ongeza maji na chumvi. Katika lita 10 za mafuta weka lita
moja ya maji na gramu 200 za chumvi. • Weka mafuta kwenye chombo cha kuchemshia
(sufuria)
• Chemsha hadi maji yote yaishe
• Sauti ya kuchemka ikiisha ni dalili kuwa maji yamekwisha.
• Ipua, acha yapoe, kisha chuja kwa kitambaa safi au chujio
• Fungasha kwenye vyombo safi na vikavu na vyenye mifuniko
• W eka lakiri na lebo • Hifadhi kwenye sehemu safi, kavu na yenye mwanga
hafifu.
MATUMIZI
Mafuta hutumika katika mapishi mbalimbali na yana
virutubishi vifuatavyo: - Mafuta gramu 100 Nguvu kilokalori 900
No comments:
Post a Comment