I DESIGNER ONE
Kichwa cha habari hapo juu ni neno la kingereza ambalo kwa lugha ya Kiswahili linamaanisha MIMI MBUNIFU.Neno hili lina maana kubwa sana.Lina maneno mawili na kwa upande wa herufi ni tisa.Nadhani wale wote ambao tunazitambua lugha mbili tu yaani Kiswahili na lugha yako ya mkoa au wilaya mpaka hapo tumeelewana.Mtu mbunifu ni yule anayeipenda kazi yake bila kujali suala la kutengeneza hela.Anapokua anafanya kazi ile kwa kutopenda ila ni kwa sababu maisha yamemshinda na kwa woga wa maisha akaamua kufanya ile kazi ili ajikwamue katika maisha basi hiyo kazi haipo toka moyoni mwake.Nilikua sipendi kufundisha ila kwa woga wa maisha nikaamua kufundisha kama ajira ya muda mfupi baada ya mipango yangu niliyopanga kukwama.Kwa hiyo ukifanya uchunguzi utagundua watu wengi wanafanya kazi ambazo hata wao hawazipendi ila tu kwa sababu hana namna ya kufanikisha kufanya kile anachokipenda.Waweza kuwa ulipenda kusomea fani Fulani ila kwa sababu hiyo fani ada yake ni ghari sana ukaamua kwenda kusoma fani nyingine.Hujaona watu wameenda kusomea fani Fulani lakini gafla wakiingia mtaani wanakutana na watu ambao hawajasoma chuo chochote ila wamejulia mtaani na wana ujuzi mkubwa kushinda wale walioenda kusomea hizo fani.Je,wanaojulia mtaani na wanakua na ujuzi mkubwa kivitendo hao ndio wana kipaji? Kama sio kipaji je hao ndio wana moyo na wameipenda hiyo fani? Wapo wengine wanafanyiwa maamuzi na wazazi wao,ndugu na jamaa zao katika maswala ya msingi.Lakini mwisho wa siku mwenye kujutia au mwenye kufurahia ule uamuzi ambao umefanyiwa ni wewe.Mtoto anapoonekana anapenda kitu Fulani ambacho kina maslahi usimuharibie na kumfayia maamuzi yako wewe kama mzazi.Mtengenezee fursa na umuwezeshe ili uweze kumjengea malengo yake katika maisha yake. Maisha ya mtu binafsi mwenye akili timamu yanatakiwa kuheshimiwa,ushauri anatakiwa kupewa mtu yeyote lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni mtu mwenyewe (I) nafsi ya kwanza na wala sio ya pili au ya tatu.Kama mzazi anapokua anaendesha maisha ya mtu na kumfanyia maamuzi ya mwisho kwa kila kitu huo ni ukandamizaji na kwa lugha ya kizungu tunasema dictatorship.Kwa wale wanaopenda kusikiliza vituo vya radio mbalimbali,channels mbalimbali hasa katika vipindi vya vijana wetu wa muziki wa bongo flavor ,tunapokuja katika swala la kuhojiwa ni nani kakusaidia hadi ukafika hapa ulipo? Wasanii wengi husema juhudi binafsi na wazazi hawakushiriki kufanikisha malengo na ndoto zake za kuwa msanii.Zaidi utasikia msanii anasema nilikua natoroka na nafanya kimya kimya na wazazi waliposikia walinigombeza na kunitaka niachane na mziki nijielekeze kusoma.Je pale msanii anapofanikiwa na mziki wake kuanza kuzalisha hela mzazi huwa anajisikiaje kwa mtoto wake pale kazi ya uhuni kwa mujibu wa wazazi inapoanza kuwatunza wazazi wake.Sikatai kusoma ni jambo la muhimu sana hata mimi nina degree.Kwa mtu uliyesoma ambae wakati upo shule ya msingi ulikua unawashinda wenzio kimasomo hadi wakakuogopa,kuna wengine uliwambia hawana akili( kwa lugha zilizozoweleka mashuleni mtu anayefeli tunasema hana akili ).Walitamani wawe kama wewe enzi hizo,walitamani uje uwakumbuke kwenye ufalme wako(maana tuliamini mtu anayefaulu vizuri na maisha kafanikiwa).Walitamani hata uje uwape kazi za kufagia ofisini mwako ukija kuwa bosi.Ulipokwenda sekondari peke yako kutoka kijijini kwako,uliwaacha wana simanzi kwa kutofanikiwa kwao.Ulipofaulu form four kwenda form five na ulipofaulu form six kwenda chuo watu walikushangaa kuwa sasa basi we ni mkombozi wa familia na kijiji chako.Umemaliza chuo ukijua kuna urahisi wa kuajiriwa na mwisho wa siku umekutana na bomu linaloweza kupasuka muda wowote.Umekutana na ulimwengu wa watanzania waliokuwa wanasoma ili waje kuajiliwa na mwisho wa siku hakuna matokeo ya kile walichokidhania au walichokitegemea wakiwa mashuleni.Wasomi sasa wamekutana na watu ambao walisoma nao shule ya msingi na wenzao japo hawajasoma wamekuwa wafanya biashara wakubwa wanamiliki nyumba na magari na pia wanaziendesha biashara vizuri kuliko hata waliosoma.Wasomi sasa wanaona aibu hata kukaa vijijini kwao kwa sababu hakuna mabadiliko yoyote zaidi ya kusema nina degree.Na kama unavojua heshima ya mtu ni pesa,pesa ni kila kitu katika maisha,shikamoo ni makelele ila pesa ndo heshima.Inauma pale unapokuwa umesomea kitu ambacho ni ngumu kukifanya kikuingizie pesa.Au pale watu wanapokuwa wamesomea vitu vinavyoweza kuingiza pesa lakini mtaji ni ndoto kuupata.Pia kuna wengine wamesomea vitu vinavyoweza kuingiza pesa wakijiajiri lakini hawako tayari kujiajiri wanasubiri kuajiriwa na wana miaka miwali au zaidi wanasambaza CV na kuendelea kukaa nyumbani kwa wazazi wao au mijini kwa kaka zao,wajomba zao baba wadogo,shangazi zao nk.Je hapo ulipo unawaza nini? Bado kuna mtu anakuwazia? Umewaza nini cha kukukwamua bado unashindwa? Unapenda kujiajiri au bado unasubiri ajira kutoka serikalini au kwenye makampuni binafsi?
Wapendwa tunatakiwa kuamka
MAKALA ZINAYOFUATA ITAJIELEKEZA KWENE MASWALI HAYA
ü Kwanini wasomi wanashindwa kufanya biashara ndodondogo zinazoweza kuzalisha kwa kiasi kikubwa?
ü Mbinu za kuweza kufanya mambo yako bila kuogopa watu wanaokuzunguka
ü Kichwa cha mwendawazimu
ü Kukopesheka kwa kijana ili kufanikisha malengo yake ya kimaisha
ü Jinsi ya kuifanya biashara yako ijulikane na ujiongezee wateja
TITO SOVELA
Phone number: 0755102156 /0655102156
Email: tsovela@gmail.com
Blog: www.idesignerone.blogspot.com
No comments:
Post a Comment